Sultan Haitham bin Tariq al Said wa Oman na Rais Vladmir Putin wa Russsia wametoa sisitizo hilo mwishoni mwa mazungumzo ya pande mbili huko Moscow.
Tamko hili la pamoja linatolewa katika hali ambayo kusisitizwa kuondoka kwa wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza na ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utatuzi wa haki wa kadhia ya Palestina kunazingatiwa kuwa ni hatua muhimu ya kupunguza mivutano na kuweka uthabiti katika eneo la Magharibi mwa Asia.
Katika taarifa hiyo ya pamoja, Rais Vladmir Putin wa Russia na Sultan Haitham bin Tariq Al Said wa Oman wamesisitiza ulazima wa kusitishwa mara moja mauaji ya raia katika Ukanda wa Gaza na kutaka kutatuliwa kwa uadilifu suala la Palestina kwa kuzingatia maslahi halali ya wananchi wa Palestina. Sehemu nyingine ya taarifa ya pamoja ya Rais wa Russia na Sultan wa Oman huko Moscow inasema: "Mwishoni mwa mazungumzo hayo, Vladimir Putin na Haitham bin Tariq Al Said walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili."
Taarifa hii inaweza kuwa ishara ya mabadiliko katika mitazamo ya kidiplomasia ya Russia na Oman katika suala la Palestina. Pia, hatua hii inaweza kuhesabiwa kuwa, juhudi za kujenga miungano mipya ya kuunga mkono haki za Wapalestina. Katika hali ambayo, nchi nyingi zinatafuta suluhu za kidiplomasia, aina hii ya ushirikiano inaweza kusaidia kuimarisha amani na utulivu katika eneo.
342/
Your Comment